Psalms 71

Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha

1 aEe Bwana, nimekukimbilia wewe,
usiache nikaaibika kamwe.
2 b cKwa haki yako uniponye na kuniokoa,
unitegee sikio lako uniokoe.
3 dUwe kwangu mwamba wa kimbilio,
mahali nitakapokimbilia kila wakati;
toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe
ni mwamba wangu na ngome yangu.
4 eEe Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu,
kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.

5 fKwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi,
tegemeo langu tangu ujana wangu.
6 gTangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,
ulinitoa tumboni mwa mama yangu.
Nitakusifu wewe daima.
7 hNimekuwa kama kioja kwa wengi,
lakini wewe ni kimbilio langu imara.
8 iKinywa changu kimejazwa sifa zako,
nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.

9 jUsinitupe wakati wa uzee,
wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.
10 kKwa maana adui zangu wananisengenya,
wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.
11 lWanasema, “Mungu amemwacha,
mkimbilieni mkamkamate,
kwani hakuna wa kumwokoa.”
12 mEe Mungu, usiwe mbali nami,
njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.
13 nWashtaki wangu na waangamie kwa aibu,
wale wanaotaka kunidhuru
na wafunikwe kwa dharau na fedheha.

14 oLakini mimi, nitatumaini siku zote,
nitakusifu zaidi na zaidi.
15 pKinywa changu kitasimulia haki yako,
wokovu wako mchana kutwa,
ingawa sifahamu kipimo chake.
16 qEe Bwana Mwenyezi, nitakuja
na kutangaza matendo yako makuu,
nitatangaza haki yako, yako peke yako.
17 rEe Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu,
hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18 sEe Mungu, usiniache,
hata niwapo mzee wa mvi,
mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho,
nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

19 tEe Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu,
wewe ambaye umefanya mambo makuu.
Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?
20 uIngawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,
utanihuisha tena,
kutoka vilindi vya dunia
utaniinua tena.
21 vUtaongeza heshima yangu
na kunifariji tena.

22 wEe Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi
kwa ajili ya uaminifu wako;
Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli,
nitakuimbia sifa kwa zeze.
23 xMidomo yangu itapaza sauti kwa furaha
ninapokuimbia sifa,
mimi, ambaye umenikomboa.
24 yUlimi wangu utasimulia matendo yako ya haki
mchana kutwa,
kwa maana wale waliotaka kunidhuru,
wameaibishwa na kufadhaishwa.
Copyright information for SwhNEN