Zechariah 13:8-9
8 akatika nchi yote,” asema Bwana,“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;
hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.
9 bHii theluthi moja nitaileta katika moto;
nitawasafisha kama fedha isafishwavyo
na kuwajaribu kama dhahabu.
Wataliitia Jina langu
nami nitawajibu;
nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’
nao watasema, ‘Bwana ni Mungu wetu.’ ”
Copyright information for
SwhNEN