1 Chronicles 26
Mabawabu
1 aHii ndiyo migawanyo ya mabawabu:Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu.
2 bMeshelemia alikuwa na wana wafuatao:
Zekaria mzaliwa wa kwanza,
Yediaeli wa pili,
Zebadia wa tatu,
Yathnieli wa nne,
3Elamu wa tano
Yehohanani wa sita
na Eliehoenai wa saba.
4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:
Shemaya mzaliwa wa kwanza,
Yehozabadi wa pili,
Yoa wa tatu,
Sakari wa nne,
Nethaneli wa tano,
5 cAmieli wa sita,
Isakari wa saba,
na Peulethai wa nane.
(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)
6Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.
9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.
10 dHosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.
12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13 eKura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.
14 fKura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. ▼
▼Shelemia jina lingine ni Meshelemia.
Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15 hKura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16 iKura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.
19 jHii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.
Watunza Hazina Na Maafisa Wengine
20 kKatika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.21 lWazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana.
23 mKutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli:
24 nShebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 25 oJamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 26 pShelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 27 qBaadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 28 rKila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.
29 sKutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.
30 tKutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 31 uKuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 32 vYeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
Copyright information for
SwhNEN