Deuteronomy 3:23-26
23 aWakati huo nilimsihi Bwana: 24 b“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 25 cAcha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.”26 dLakini kwa sababu yenu Bwana alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Bwana aliniambia, “Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena.
Copyright information for
SwhNEN