Ecclesiastes 12:1-7
1 aMkumbuke Muumba wakosiku za ujana wako,
kabla hazijaja siku za taabu,
wala haijakaribia miaka utakaposema,
“Mimi sifurahii hiyo”:
2kabla jua na nuru,
nao mwezi na nyota havijatiwa giza,
kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
3 bsiku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka,
nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha,
wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache,
nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
4 cwakati milango ya kuingia barabarani itakapofungwa
na sauti ya kusaga kufifia;
wakati watu wataamshwa kwa sauti ya ndege,
lakini nyimbo zao zote zikififia;
5 dwakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu
na hatari zitakazokuwepo barabarani;
wakati mlozi utakapochanua maua
na panzi kujikokota
nawe usiwe na shauku ya kitu chochote.
Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele
nao waombolezaji wakizunguka barabarani.
6Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha,
au bakuli la dhahabu halijavunjika;
kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi,
au gurudumu kuvunjika kisimani,
7 enayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka,
na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
Copyright information for
SwhNEN