Exodus 12:23-27
23 aBwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi.24“Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. 25 bMtakapoingia katika nchi Bwana atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. 26 cWatoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ 27 dBasi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Bwana, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu.
Copyright information for
SwhNEN