Isaiah 13:19-22
19 aBabeli, johari ya falme,utukufu wa kiburi cha Wababeli, ▼
▼Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo.
itaangushwa na Mungu
kama Sodoma na Gomora.
20 cHautakaliwa na watu kamwe
wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote.
Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,
hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko.
21 dLakini viumbe wa jangwani watalala huko,
mbweha watajaza nyumba zake,
bundi wataishi humo
nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.
22 eFisi watalia ndani ya ngome zake,
mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari.
Wakati wake umewadia,
na siku zake hazitaongezwa.
Copyright information for
SwhNEN