Isaiah 66:1-2
Hukumu Na Matumaini
1 aHili ndilo asemalo Bwana,“Mbingu ni kiti changu cha enzi,
nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.
Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?
Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?
2 bJe, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,
hivyo vikapata kuwepo?”
asema Bwana.
“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:
yeye ambaye ni mnyenyekevu
na mwenye roho yenye toba,
atetemekaye asikiapo neno langu.
Copyright information for
SwhNEN