Isaiah 8:8-10
8 ana kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake,yakipita katikati na yakifika hadi shingoni.
Mabawa yake yaliyokunjuliwa
yatafunika upana wa nchi yako,
Ee Imanueli!” ▼
▼Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.
9 cInueni kilio cha vita, enyi mataifa,
na mkavunjwevunjwe!
Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
10 dWekeni mikakati yenu, lakini itashindwa;
fanyeni mipango yenu, lakini haitafanikiwa,
kwa maana Mungu yu pamoja nasi. ▼
▼Kiebrania ni Imanueli.
Copyright information for
SwhNEN