Nehemiah 13:10-12
10 aPia niligundua kuwa mafungu yaliyopangwa kupewa Walawi hawakuwa wamepewa, nao Walawi wote na waimbaji waliowajibika kwa huduma walikuwa wamerudi katika mashamba yao. 11 bBasi niliwakemea maafisa na kuwauliza, “Kwa nini nyumba ya Mungu imepuuzwa?” Kisha niliwaita pamoja na kuwaweka kwenye nafasi zao.12 cYuda wote walileta zaka za nafaka, divai mpya na mafuta kwenye ghala.
Copyright information for
SwhNEN