e1Sam 3:7, 21; Mwa 15:1; 20:3; 46:2; Mt 27:19; Ebr 1:1; 1Fal 3:5; Mwa 46:2; Ay 33:15; Lk 1:11; 1:22; Mt 1:20
Numbers 12
Miriamu Na Aroni Wampinga Mose
1 aMiriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 bWaliuliza, “Je, Bwana amesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye Bwana akasikia hili.3 c(Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)
4Ghafula Bwana akawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda. 5 dKisha Bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele, 6 eBwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu:
“Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.
7 fLakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;
yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
8 gKwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Bwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”
9 hHasira ya Bwana ikawaka dhidi yao, akawaacha.
10 iWakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia, akaona ana ukoma. 11 jKisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu. 12 kUsimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”
13 lHivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”
14 m Bwana akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” 15 nKwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.
16 oBaada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.
Copyright information for
SwhNEN