Proverbs 11
1 a Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,bali vipimo sahihi ni furaha yake.
2 bKiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,
bali unyenyekevu huja na hekima.
3 cUadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
4 dUtajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini.
5 eHaki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
6 fHaki ya wanyofu huwaokoa,
bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
7 gWakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka;
yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
8 hMtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu,
naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
9 iKwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu
humwangamiza jirani yake,
bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
10 jWakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;
mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
11 kKutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,
bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
12 lMtu asiye na akili humdharau jirani yake,
bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
13 mMasengenyo husaliti tumaini,
bali mtu mwaminifu hutunza siri.
14 nPasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,
bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
15 oYeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka,
bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
16 pMwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima,
bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
17 qMwenye huruma hujinufaisha mwenyewe,
bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
18 rMtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,
bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
19 sMtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima,
bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.
20 t Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu,
bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
21 uUwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa,
bali wenye haki watakuwa huru.
22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe
ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.
23 vShauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,
bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.
24 wKuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,
mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
25 xMtu mkarimu atastawi;
yeye awaburudishaye wengine
ataburudishwa mwenyewe.
26 yWatu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,
bali baraka itamkalia kichwani kama taji
yeye aliye radhi kuiuza.
27 zYeye atafutaye mema hupata ukarimu,
bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
28 aaYeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,
bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
29 abYeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,
naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
30 acTunda la mwenye haki ni mti wa uzima,
naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
31 adKama wenye haki watapokea ujira wao duniani,
si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?
Copyright information for
SwhNEN