Proverbs 2
Faida Za Hekima
1 aMwanangu, kama utayakubali maneno yanguna kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
2 bkutega sikio lako kwenye hekima
na kuweka moyo wako katika ufahamu,
3 cna kama ukiita busara
na kuita kwa sauti ufahamu,
4 dna kama utaitafuta kama fedha
na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
5 endipo utakapoelewa kumcha Bwana
na kupata maarifa ya Mungu.
6 fKwa maana Bwana hutoa hekima,
na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7 gAnahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,
yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
8 hkwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki
na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
9 iNdipo utafahamu lipi lililo kweli na haki
na sawa: yaani kila njia nzuri.
10 jKwa maana hekima itaingia moyoni mwako,
nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
11 kBusara itakuhifadhi
na ufahamu utakulinda.
12 lHekima itakuokoa kutoka njia za waovu,
kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,
13 mwale waachao mapito yaliyonyooka
wakatembea katika njia za giza,
14 nwale wapendao kutenda mabaya
na kufurahia upotovu wa ubaya,
15 oambao mapito yao yamepotoka
na ambao ni wapotovu katika njia zao.
16 pItakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,
kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno
ya kushawishi kutenda ubaya,
17 qaliyemwacha mwenzi wa ujana wake
na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.
18 rKwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo
na mapito yake kwenye roho za waliokufa.
19 sHakuna yeyote aendaye kwake akarudi,
au kufikia mapito ya uzima.
20 tHivyo utatembea katika njia za watu wema
na kushikamana na mapito ya wenye haki.
21 uKwa maana wanyofu wataishi katika nchi,
nao wasio na lawama watabakia ndani yake.
22 vBali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi,
nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.
Copyright information for
SwhNEN