Psalms 73

KITABU CHA TATU

(Zaburi 73–89)

Haki Ya Mungu

Zaburi ya Asafu.

1 aHakika Mungu ni mwema kwa Israeli,
kwa wale ambao mioyo yao ni safi.

2 bBali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza;
nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.
3 cKwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna
nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

4Wao hawana taabu,
Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao.

miili yao ina afya na nguvu.
5 eHawapati shida zinazowataabisha watu wengine,
wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.
6 fKwa hiyo kiburi ni mkufu wao,
wamejivika jeuri.
7 gUovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi,
majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.
8 hHudhihaki na kusema kwa ukorofi,
katika majivuno yao wanatishia kutesa.
9 iVinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu,
nazo ndimi zao humiliki duniani.
10Kwa hiyo watu wao huwageukia
na kunywa maji tele.
Au: na kupokea yote wasemayo.

11 kWanasema, “Mungu awezaje kujua?
Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”

12 lHivi ndivyo walivyo waovu:
siku zote hawajali,
wanaongezeka katika utajiri.

13 mHakika nimeuweka moyo wangu safi bure,
ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.
14 nMchana kutwa nimetaabika,
nimeadhibiwa kila asubuhi.

15Kama ningesema, “Nitasema hivi,”
ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.
16 oNilipojaribu kuelewa haya yote,
yalikuwa magumu kwangu kuelewa.
17 pMpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu,
ndipo nilipotambua mwisho wao.

18 qHakika unawaweka mahali pa utelezi,
unawaangusha chini kwa uharibifu.
19 rTazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula,
wanatoweshwa kabisa na vitisho!
20 sKama ndoto mtu aamkapo,
hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana,
utawatowesha kama ndoto.

21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa,
na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22 tnilikuwa mpumbavu na mjinga,
nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.

23 uHata hivyo niko pamoja nawe siku zote,
umenishika mkono wangu wa kuume.
24 vUnaniongoza kwa shauri lako,
hatimaye utaniingiza katika utukufu.
25 wNani niliye naye mbinguni ila wewe?
Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
26 xMwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,
bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu
na fungu langu milele.

27 yWale walio mbali nawe wataangamia,
unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
28 zLakini kwangu mimi,
ni vyema kuwa karibu na Mungu.
Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu;
nami nitayasimulia matendo yako yote.
Copyright information for SwhNEN