Song of Solomon 8

1 aLaiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa kiume,
ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!
Kisha, kama ningekukuta huko nje,
ningelikubusu,
wala hakuna mtu yeyote angelinidharau.
2Ningelikuongoza na kukuleta
katika nyumba ya mama yangu,
yeye ambaye amenifundisha.
Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,
asali ya maua ya mikomamanga yangu.
3 bMkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
4 cBinti za Yerusalemu, ninawaagiza:
msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Sita

Marafiki

5 dNi nani huyu anayekuja kutoka nyikani
akimwegemea mpenzi wake?
Mpendwa

Nilikuamsha chini ya mtofaa,
huko mama yako alipotunga mimba yako,
huko yeye alipata utungu akakuzaa.
6 eNitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri kwenye mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama kuzimu.
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa.
7 fMaji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
mito haiwezi kuugharikisha.
Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwake
kwa ajili ya upendo,
angelidharauliwa kabisa.
Marafiki

8Tunaye dada mdogo,
matiti yake hayajakua bado.
Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu
wakati atakapokuja kuposwa?
9Kama yeye ni ukuta,
tutajenga minara ya fedha juu yake.
Na kama yeye ni mlango,
tutamzungushia mbao za mierezi.
Mpendwa

10 gMimi ni ukuta,
nayo matiti yangu ni kama minara.
Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake
kama yule anayeleta utoshelevu.
11 hSolomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;
alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.
Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake
shekeli 1,000
Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5.
za fedha.
12Lakini shamba langu la mizabibu
ambalo ni langu mwenyewe
ni langu kutoa;
hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni,
na shekeli mia mbili
Shekeli 200 ni kama kilo 2.3.
ni kwa ajili
ya wale wanaotunza matunda yake.
Mpenzi

13 kWewe ukaaye bustanini
pamoja na marafiki mliohudhuria,
hebu nisikie sauti yako!
Mpendwa

14 lNjoo, mpenzi wangu,
uwe kama swala
au kama ayala kijana
juu ya milima iliyojaa vikolezo.
Copyright information for SwhNEN