Job 19

Hotuba Ya Sita Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai

1Ndipo Ayubu akajibu:

2 a“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini,
na kuniponda kwa maneno yenu?
3 bMara kumi hizi mmenishutumu;
bila aibu mnanishambulia.
4 cKama ni kweli nimepotoka,
kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.
5 dKama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu,
na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,
6 ebasi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya,
naye amekokota wavu wake kunizunguka.

7 f“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu;
ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
8 gYeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita;
ameyafunika mapito yangu na giza.
9 hAmenivua heshima yangu,
na kuniondolea taji kichwani pangu.
10 iAmenibomoa kila upande hadi nimeisha;
amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
11 jHasira yake imewaka juu yangu;
amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
12 kMajeshi yake yananisogelea kwa nguvu;
yamenizingira,
yamepiga kambi kulizunguka hema langu.

13 l“Amewatenga ndugu zangu mbali nami;
wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
14 mWatu wa jamaa yangu wamekwenda mbali;
rafiki zangu wamenisahau.
15 nWageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni;
wananitazama kama mgeni.
16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki,
ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
17 oPumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu;
nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
18 pHata watoto wadogo hunidhihaki;
ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
19 qRafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;
wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
20 rMimi nimebaki mifupa na ngozi tu;
nimeponea nikiwa karibu kufa.

21 s“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma,
kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
22 tKwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo?
Hamtosheki kamwe na mwili wangu?

23 u“Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu,
laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,
24 vkwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma,
au kuyachonga juu ya mwamba milele!
25 wNinajua kwamba Mkombozi
Au: Mtetezi.
wangu yu hai,
naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
26 yNami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,
bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
27 zmimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe:
mimi, wala si mwingine.
Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!

28“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda,
maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’
29 aaninyi wenyewe uogopeni upanga,
kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga,
nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”
Copyright information for SwhNEN