Psalms 32
Furaha Ya Msamaha
Zaburi ya Daudi. Funzo.
1 aHeri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,ambaye dhambi zake zimefunikwa.
2 bHeri mtu yule ambaye Bwana
hamhesabii dhambi,
na ambaye rohoni mwake
hamna udanganyifu.
3 cNiliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa
kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.
4 dUsiku na mchana
mkono wako ulinilemea,
nguvu zangu zilinyonywa
kama vile katika joto la kiangazi.
5 eKisha nilikujulisha dhambi yangu
wala sikuficha uovu wangu.
Nilisema, “Nitaungama
makosa yangu kwa Bwana.”
Ndipo uliponisamehe
hatia ya dhambi yangu.
6 fKwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe
wakati unapopatikana,
hakika maji makuu yatakapofurika
hayatamfikia yeye.
7 gWewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,
utaniepusha na taabu
na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.
8 hNitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
nitakushauri na kukuangalia.
9 iUsiwe kama farasi au nyumbu
wasio na akili,
ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu
la sivyo hawatakukaribia.
10 jMtu mwovu ana taabu nyingi,
bali upendo usio na kikomo wa Bwana
unamzunguka mtu anayemtumaini.
11 kShangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki!
Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!
Copyright information for
SwhNEN